Alichokiona Afande Sele Baada ya Kufika Coco Beach ya Dar

Msani wa miondoko ya Rap kutoka mro ambaye alikuwa Mgombea wa Ubunge jimbo la Morogoro mjini  ameshangazwa hali ambayo ameikuta katika fukwe ya Coco Beach Wikendi ya leo na kutoa ya moyoni kuhusu hali aliyoiona.


Alichandika kupitia akaunti yake ya Facebook kuhusu hali katika fukwe ya Coco Beach

Nimefika coco beach nimekoma mwenyewe😳...zile mbwembwe za watu wa dar kufurika kila jpili kama leo kula bata zakuzidi zimekwisha kabisa😌...nilichoshuhudia ni wahudumu,chinga,wamasai wenye bidhaa zisizokua na wateja,ombaomba wakila rika na kila jinsia na wenzangu namimi wachache ambao wengi wetu tunazugazuga tu labda fahari yetu ya macho ni kuangalia bahari (hasa kwa mshamba kama mimi wa moro)na wazungu wanaokula,kunywa na kusaza kama enzi za ukoloni...🚶🏿...narudi zangu moro sasa nikale zangu maembe tu kwani msimu ndio huu...🖐🏿