Maombi dhamana ya Lema kuwasilishwa leo

Arusha, Mawakili wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambaye yupo mahabusu ya Gereza Kuu la Kisongo, jana walishindwa kukamilisha utaratibu wa kisheria wa kuwasilisha maombi ya dhamana Mahakama Kuu.

Akizungumza na Mwananchi wakili wa mshtakiwa huyo, John Mallya alisema watawasilisha maombi hayo leo wakati wa kusikilizwa kesi nyingine za mteja wao. “Bado kuna utaratibu unaendelea, tunatarajia kesho (leo) tutaukamilisha,” alisema Mallya.

#Mwananchi