Alichandika Nisha Bebee baada ya Watu kumkejeli kwenye mtandao, baada ya kupost kuwa amebakwa na kupata Mimba
Wengi waliniona kama napost vitu vya ndani kwanini mwanzo sikusema,kikubwa nilikuwa natamani amani ya moyo wangu,kukaa na kitu rohoni kikakutesa inauma zaidi.KUSEMA UKWELI imenipa amani na kurudisha asilimia kadhaa za furaha moyoni mwangu.
#KUBAKWA ni neno kubwa sana kuitamka kwenye watu wengi kiasi hiki,ila wengi wetu tumekuwa tukibakwa na waume zetu/boyfriends/girlfriend bila kulijua hilo.
#KUBAKWA ni kitendo cha kuingiliwa kimwili bila ridhaa yako,wangapi mmegombana na wapenzi wenu mwisho wa siku wakawaingilia ugomvi ukaisha?? huwa tunaona kawaida ila wenzetu wazungu hiyo ni kubakwa na unashtakiwa.
Kinachoniuma zaidi kuwa na mtoto wa baba ambaye hatujakubaliana hilo,ndio maana inafika hatua nashindwa jizuia hisia zangu,ndio aliwahi kuwa boyfriend wng tatizo ni mkataba wetu ulishaisha,nishalia sana..nishaumia sana..ila nimepokea ushauri wenu.
Wengi wamenikejeli ahsante,wapo walonipa pole, ahsanteni,na wapo pia walonishauri mabaya na mazuri,ushauri mkubwa kwangu ni kuyaacha haya yapite na kuganga yajayo kwani mm si wa design hii. Mlotoa hili wale wa #dm whatsapp na page zenu.. mmefanikiwa kunirudisha nawashukuru sanaaa.
Mlonishauri #KUTOAMIMBA Mungu anawaona,huyu ni wangu sitomtoa kama aliingia kwangu naamini ilishaandikwa hivyo,wangapi wanalilia watoto hawawapati.. thanx kwa everything... mnaonambia mimba yangu imemchukia baba pia sawa. BYE