RIDHIWANI KIKWETE: Mimi ni tajiri wa Marafiki, Sina Maghorofa wala vituo vya Mafuta

Katika hatua nyingine Mbunge huyo amekanusha uvumi unaoenea mitaani kwamba yeye ni tajiri na anamiliki mali nyingi nchini. “Mimi ni tajiri wa Marafiki sio mali, ni porojo tu ninachomiliki kinanitosha mimi na ndugu zangu, sina Maghorofa wala vituo vya mafuta” Alimaliza Mh Kikwete.



Mbunge wa jimbo la Chalinze ambaye pia ni Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Ridhiwan Kikwete amesema urafiki kati ya baba yake na aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa bado upo na wanawasiliana kwenye simu mara kwa mara.

Akiongea kupitia kipindi cha Sun Rise cha Times Fm mapema leo asubuhi, Ridhiwan amedai kuna watu ambao kazi yao ni ‘Kupika’ habari ndio wanaopotosha umma lakini mahusiano ni mazuri kati ya viongozi hao wastaafu. “Lowassa na Kikwete ni Marafiki mpaka Kesho wanasalimiana, kumekuwa na upishi tu wa Habari, ukweli ni kwamba mambo ni mazuri” Alisema.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo amekanusha uvumi unaoenea mitaani kwamba yeye ni tajiri na anamiliki mali nyingi nchini. “Mimi ni tajiri wa Marafiki sio mali, ni porojo tu ninachomiliki kinanitosha mimi na ndugu zangu, sina Maghorofa wala vituo vya mafuta” Alimaliza Mh Kikwete. 

Pia amezungumzia kuhusu Maendeleo ya Jimbo lake Chalinze kuhusu miradi ya Maji. "Tumeanza kuchimba Visima, tumeshachimba 10 tayari,na tunaelekea kwenye mradi mkubwa wa Wami" Alisema

Katika Masuala ya Michezo katika Jimno lake Ridhiwani anasema  'Tunashida ya Mipango kwenye michezo, mfano wachezaji wengi wa Chalinze si Wazawa' . Vile vile aligusia kuhusu Suala la Yanaga na Kusema  'Si Busara kuingiza Pua katika Biashara isiyo kuhusu, Leo hii nilikuwa nategemea Watanzania wapige kelele kwa klabu kama ya Yanga wachezaji Wazawa wanawekwa Benchi' Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwan Kikwete.