Moshi. Vilio na simanzi juzi vilitawala katika kitongoji cha Kichari, Kijiji cha Umbwe Onana wilayani Moshi baada ya watoto yatima tisa kuondolewa kwa amri ya Mahakama kwenye nyumba ya marehemu baba yao waliyokuwa wakiishi.
Hali hiyo ilisababisha wakazi wa kijiji hicho kuamua kupiga kambi barabarani wakimuomba Mungu atende miujiza kwa yatima hao.
Wananchi hao wakiongozwa na baadhi ya viongozi wa dini, waliliambia gazeti la mwananchi kuwa watapiga kambi na kufanya maombi maalumu ya siku tisa kuwaombea watoto hao waliotolewa kwenye nyumba hiyo.
#Mwananchi