MWANAMKE TAJIRI BARANI AFRIKA

Mwanamke tajiri zaidi barani Afrika Isabel dos Santos, bintiye rais wa Angola, amejiongezea utajiri baada ya kuchukua udhibiti wa benki kubwa zaidi nchini humo. Bi Santos amechukua udhibiti wa benki hiyo ya BFA baada ya kampuni yake kununua hisa zaidi katika benki hiyo na kudhibiti zaidi ya asilimia 50 ya hisa katika benki hiyo.

Hatua hiyo imewaacha waangalizi kutojua ikiwa watamshangilia mama huyu mjasiria mali au kulalamikia mamlaka na ushawishi wa kiuchumi walio nao matajiri wachache sana barani afrika.

Isabel dos Santos mwenye umri wa miaka 43, amefanikiwa na angali na ari ya kufanikiwa zaidi katika kanda ambayo wanaume wanatawala katika ofisi nyingi za umma na za kibinafsi. Bi Dos Santos, ni bintiye rais wa angola Jose Eduardo dos Santos, ambaye ameongoza taifa hilo tangu mwaka wa elfu moja mia kenda na sabini na tisa. Angola ni moja ya mataifa masikini zaidi duniani.

#BBC