KWESI APPIAH ATEULIWA KUWA KOCHA MKUU GHANA


Chama cha soka cha Ghana kimemteua tena Kwesi Appiah kuwa kocha mkuu wa wa timu ya taifa ya Ghana Black stars.

Appiah amepewa mkataba wa miaka miwili wa kuinoa timu ya taifa na ataanza kazi yake rasmi mwezi mei mwaka huu.

Kocha huyu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Avram Grant ambaye alijiuzulu baada ya kumalizika kwa fainali za michuano ya kombe la mataifa ya afrika ya mwaka 2017.

Hii ni mara ya pili kwa kocha huyu kuinoa timu hiyo taifa mara ya kwanza aliiongoza timu hiyo kuanzia mwaka 2012 mpaka 2014