MAREKANI YAELEKEZA MASHAMBULIZI YA MAKOMBORA KWENYE ANGA LA SYRIA

Usiku wa kuamkia leo Marekani yashambulia kwa makombora 59 ya kijeshi yaliyoelekezwa katika ngome ya Jeshi la anga la Syria.

Mashambulizi hayo yametekelezwa kutoka kwenye meli za kijeshi za Marekani katika bahari ya Mediterranea.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema ameamuru kutekelezwa kwa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Syria huku akitoa wito kwa mataifa yote yaliyostaarabika kukomesha vitendo vya mauaji na umwagaji damu nchini humo

Naye mshirika wa Syria, Urusi ametahadharisha madhara yatokanayo na hatua zozote za kijeshi zinazochukuliwa na Marekani dhidi ya Syria .k