MIAKA MITANO BAADA YA KIFO CHA KANUMBA


Ikiwa leo ni Miaka 45 tangu alipofariki Dunia mwanamapinduzi na muasisi wa taifa la Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume leo pia ni miaka 5 tangu alipofariki Dunia msanii mashuhuri wa filamu nchini Steven Kanumba

Kanumba alifariki siku ya Jumatatu mwaka 2012 akiwa nyumbani kwake Sinza Vatican na chanzo cha kifo chake kama kilivyothibitishwa na aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni wakati huo Charles Kenyela ilikuwa ni Ugomvi baina yake na mpenzi wake wakiwa ndani ya nyumba hiyo

Taarifa za kifo cha Kanumba zilianza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na hakukuwa na mpenzi wa filamu ambaye aliweza kuamini kuwa Kanumba amefariki dunia, Mazishi yake yalifanyika katika makaburi ya Kinondoni  siku tatu baada ya kifo chake yaani Tarehe 10

Kanumba alifanikiwa kuigiza filamu nyingi na baadhi ya filamu zilizowahi kumpa umaarufu Kanumba ni Uncle JJ,This Is It,Ndoa ya yangu,Love and Power,Dar to Lagos na nyingine nyingi

Je Ni Movie Gani ya Marehemu Kanumba ilikuwa inakuvutia sanaa