ETHIOPIA: Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amezindua jumba la Makao Makuu ya Umoja wa Afrika lililopewa jina la Mwalimu Julius Nyerere.



Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani.

Litakuwa Makao Makuu ya Idara ya Amani na Usalama ya Umoja wa Afrika na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani Afrika pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani.