MASABURI KUZIKWA CHANIKA JUMATATU



Mazishi ya aliyekuwa Meya wa jiji hili Didas Masaburi yanatarajiwa kufanyika jumatatu Chanika ndani ya eneo la chuo alichokuwa akikimiliki. Masaburi alifariki usiku wa kuamkia leo  akiwa na umri  wa miaka 56.  Ameacha wake watatu na watoto 17.

Kwa mujibu wa mtoto wake wa kwanza Steven Masaburi amesema baba yake alifariki jana saa mbili usiku lakini wakati wa uhai wake alikuwa akisema mara kadhaa kwamba siku akifariki azikwe katika eneo hilo "Mzee alikuwa ni mtu wa matani sana lakini siku zote alikuwa akisema akifariki azikwe katika eneo hili ambalo alikuwa akitumia muda mwingi kujitaftia riziki" Aliwahi kuwa Meya wa Dar es Salaam mwaka 2010- 2015 na mgombea ubunge wa CCM mwaka 2015 katika jimbo la Ubungo.