Anakuwa mtangazaji wa pili wa EFM kuchukuliwa na Clouds katika kipindi cha mwezi mmoja, baada ya Kicheko.
PJ aliyeondoka Clouds mwanzoni mwa mwaka huu akiwa na Gerald Hando, ametambulishwa rasmi Jumatano hii.
Anamfuata mtangazaji mwingine aliyehama Clouds akaenda EFM na kisha kurejea tena kwenye kituo hicho, Gardiner G Habash.
Mtangazaji huyo anayesifika kwa uhodari wa kuchambua magazeti, alikuwa na mchango mkubwa wa kukifanya kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM kujipatia umaarufu ndani ya muda mfupi.
Kupokonywa kwa PJ EFM kunachochea zaidi uhasama kati yake na Clouds FM.