Maneno ya Mwigulu Nchemba, Roma Mkatoliki na Lulu kuhusu mwanafunzi Aliyepigwa kama mwizi



Maneno ya Mwigulu Nchemba Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba tukio hili limetokea Mbeya Sekondari.Wahusika ni Waalimu waliokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo (Field). Waziri amewaagiza watendaji wa Wizara yake Mkoani Mbeya wafuatilie. 


Maneno ya Roma Mkatoliki
#KunaWanafunzi_ni_wakorofi
#Kuliko_mnavyoweza_kufikiria
Lakini Hata kama Huyu mwanafunzi
#KAUA#KABAKA#KAIBA#KATONGOZA
#MWALIMU#ANAPIGA_WENZAKE etc.
Mfahamu kuwa
Tuliposema Ualimu ni #Wito
Tulimaanisha  kuifata na kuiishi misingi na maadili ya kazi hiyo.
Mimi kama Mzazi na Kama mwalimu  NASEMAJE
#HILI_HALIKUBALIKI
#HILI_HALIKUBALIKI
Walimu wenzangu nisaidieni hapa hawa walimu wenzetu wako sahihi?. Au labda wanaweza kutushawishi wakitupa sababu ya kosa la mwanafunzi huyo!!! Naamini hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao!! 

Maneno ya Lulu (Elizabeth Michael)

Kilichonisikitisha Zaidi NI sauti ya Mwanamke anayetetea na ku support huyo mwanafunzi anavyopigwa...Mwanamke ambaye pengine ni mama tayari au mama mtarajiwa😪Hii Si Sawa....hatutetei makosa lakini upigaji wa aina hii sio suluhisho la hayo Makosa....zitafutwe adhabu sahihi..!!!