Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameshiriki na wakazi katika shughuli za kila siku

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekuwa akizuru maeneo ya mashambani na kushiriki na wakazi katika shughuli za kila siku, chini ya anachosema ni Operesheni ya Kuunda Mali.




Katika siku ya tatu, aliteka maji na kuyasafirisha kwa baiskeli kuwaonyesha wakazi juu ya teknolojia ya unyunyiziaji mashamba maji ya tone kwa tone shambani. Amefanya hivyo katika shamba la ekari 24 lililo Kawumu, wilayani Luweero katikati mwa nchi hiyo. “Nitaendelea kuwahamasisha wakazi nyumba hadi nyumba kupitia Operesheni ya Kuunda Mali,” amesema.