TANZIA: BONDIA THOMAS MASHARI

BONDIA THOMAS  MASHARI ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo kwa taarifa zaidi ungana NASI 



Mashali aliyezaliwa kwa jina Christopher Fabian Mashale aliuawa baada ya kupigwa akiwa huko Kimara jijini Dar es Salaam. Inasemekana wakati akinywa pombe, ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye anadaiwa kupiga kelele kusema Mashali ni mwizi na watu kuanza kumshambulia.

Ndugu zake wanadai kuwa walimkuta akivuja damu nyingi. Taarifa zinadai kuwa alipelekwa katika hospitali ya Sinza Palestina kabla ya kupelekwa Muhimbili ambako mauti ilimkuta. Inasemekana kuwa hadi jioni alikuwa na bondia mwenzake, Francis Cheka.

Chanzo: Bongo5