DR. LICKY ABDALLAH AWATUMBUA JIPU AZAM TV



Mchambuzi wa soka nchini anayeheshimika kwa uchambuzi makini kwenye ngazi zote za kitaifa na kimataifa, akichambua bila upendeleo wala kupepesa macho, huku akijikita kwenye uhalisia zaidi, Licky Abdallah, maarufu kama Dr. Licky amewasulubu na kuwaponda warusha matangazo wa Azam TV kwamba wanakuza matukio kwa kuchezesha na kuchelewesha camera zao, na kuwachonganisha waamuzi wa mpira kwa Bodi ya Ligi.

Amefafanua kwamba, ameangalia mechi zote za Simba SC na Young Africans weekend hii, na kugundua kwamba kila Yanga wanapofunga goli, wana-scroll camera zao ili ioneshe wameotea, hivyo kusababisha na kusambaza upotoshaji mkubwa kwa umma.

Amesema ujanja huo amefafanuliwa na rafiki yake ambaye anaonesha matangazo ya Ligi Kuu ya Uingereza, kupitia TV1.