Kituo cha ugunduzi wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kutumia panya buku kimezinduliwa leo (Jumatano) jijini Dar es Salaam. Kituo hicho cha pili kwa Tanzania kinaratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la Apopo lenye makao makuu nchini Ubelgiji.
Panya kwa ajili ya Utafiti |
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho Meneja wa mpango huo nchini, Dk Georgies Mgode amesema panya hao wanasaidia kugundua ugonjwa wa kifua kikuu ndani ya muda mfupi.
Amesema tangu panya hao wameanza kufanya kazi wamefanikiwa kugundua wagonjwa 10000 ambao vipimo vya hospitali vilishindwa kugundua.
#Mwananchi