MASWALI 20 KUHUSU JPM NA TUZO ZA "FORBES POY2016"

By Malisa GJ,



Zikiwa zimesalia siku 14 tu kabla ya kutolewa kwa Tuzo ziitwazo "Forbes Africa Person of the Year2016" kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya tuzo hizo. Mjadala huu umegawanyika makundi mawili. Kuna wanaosema tuzo hizi "Hazipo" na wanaosema "Zipo". Lakini makundi yote mawili hayajaweza kujadili kwa undani kuhusu tuzo hizi. Wote wameng'ang'ania kuwepo au kutokuwepo kwa tuzo hizi na uhusiano wake na jarida la "Forbes" la nchini Marekani, na hawakwenda zaidi ya hapo.

Kwa hiyo mjadala huo umeacha maswali mengi kwa jamii ambayo hayana majibu. Leo ningependa kuangazia maswali 20 muhimu, ili kila mmoja aweze kujua kuhusiana na tuzo hizi. Kwahiyo leo natoa shule kidogo (bila ada).

#SWALI_No1: Je tuzo za "Forbes Africa POY" zipo au hazipo?
JIBU: Zipo.

#SWALI_No2: Je kilele cha tuzo hizo mwaka huu kinafanyikia wapi, na lini?
JIBU: Kilele kitakuwa mjini Nairobi, nchini Kenya tarehe 27 November mwaka huu.

#SWALI_No3: Je tuzo hizi zinatolewa na jarida  Forbes la nchini Marekani?
JIBU: Hapana. Jarida la "Forbes" halihusiki kwa vyovyote katika uandaaji wala utoaji wa tuzo hizi.

#SWALI_No4:Tuzo hizi zinadhaminiwa/fadhiliwa na nani?
JIBU: Tuzo hizi zina wadhamini wakuu watatu. Mosi ni "Bank M", pili ni kampuni ya magari ya Jaguar na tatu ni kampuni ya magari ya LandRover.

#SWALI_No5: Tuzo hizi zinaandaliwa na kutolewa na nani?
JIBU: Tuzo hizi zinaandaliwa na kutolewa na kampuni ya ABN Event production au ABN360 ya nchini Afrika Kusini, yenye makao yake mjini Sandton, jengo la West Tower, ghorofa ya 4. Tovuti yao ni http://poy2016.com/

#SSWALI_No6: ABN Event Production ni nini?
JIBU: NI kampuni ya uandaaji wa matukio mbalimbali (event production company) kama vile semina, makongamano, warsha na mikutano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Hawana tofauti sana na "Pilipili Production" ile ya MC Pilipili, au "Watanashati Production" ya McDouble A. Ukiwa na tukio lako kama vile Kongamano, mkutano au sherehe unawatajia bajeti yako then wao wanakusaidia kuandaa kila kitu.
Hadi sasa wameshandaa makongamano mengi ya kimataifa likiwemo kongamano la dunia la masuala ya UKIMWI (The 21st International AIDS conference) lililofanyika mjini Durban,nchini Afrika Kusini (http://www.aids2016.org/Media-Centre/The-Latest/Press-Releases/ArticleID/14/The-21st-International-AIDS-Conference-to-take-place-on-18-22-July-2016).

#SWALI_No7: Je kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya jarida la Forbes la nchini Marekani na kampuni ya ABN Event Production ya waandaaji wa tuzo za Forbes Africa Person of the Year?
JIBU: kuna uhusiano lakini si wa moja kwa moja. Jarida la Forbes si mmiliki wala sehemu ya wamiliki wa kampuni ya ABN Event Production ya nchini Afrika Kusini.

#SWALI_No8: Jarida la Forbes huzalishwa na nani?
JIBU: Jarida la Forbes huzalishwa na kampuni ya Forbes Inc, yenye makao yake makuu mjini New Jersey, nchini Marekani. Jarida hili linamilikiwa na Bilionea wa kimarekani aitwae Steve Forbes ambaye pia ndio Editor-In-Chief wa jarida hilo. Tovuti rasmi ya jarida ya "Forbes" ni http://www.forbes.com/

#SWALI_No09: Jarida la Forbes lina tuzo zozote ziitwazo "Forbes Africa Person of the Year?"
JIBU: Hapana. Jarida la Forbes halina tuzo za aina hiyo na halijawahi kutoa tuzo zenye jina kama hilo au linalofanana na hilo. Jarida hili ni maarufu kwa kutoa orodha mbalimbali za watu mashuhuri. Kwa mfano orodha ya matajiri wa Marekani (Forbes 400), orodha ya makampuni makubwa zaidi duniani (Forbes Global 2000), orodha ya watu matajiri zaidi duniani (Forbes the World's Bilionaires) etc. Jarida la Forbes halina kitu kinachoitwa "Forbes Person of the Year Award".

#SWALI_No10: Kwanini kampuni ya ABN360 inatumia jina "Forbes" kwenye tuzo zake za "African Person of the Year?"
JIBU: Mwaka 2011 mwezi November, kampuni ya ABN ilibuni tuzo hizi lakini haikuweza kuzitengenezea "credibility" kwa muda mfupi. Kwahiyo wakaingia mkataba maalumu na kampuni ya "Forbes Inc" ya nchini Marekani (wachapishaji wa jarida la Forbes) kuhusu kutumia "identity" ya Forbes ili kuongeza credibility katika tuzo hizo.

Kampuni ya ABN360 ilikubali kuilipa "Forbes Inc" kiasi kadhaa cha pesa ili kuweza kutumia jina "Forbes" kwenye tuzo zao. Makubaliano hayo yanaambatana na kutumia coorporate IDs zote ikiwa ni pamoja na corporate colour, logo, slogan, signature and anyother sign alligned with Forbes Inc. Sehemu ya mkataba huo iko hapa  http://www.forbesaust.com.au/Conditions.

#SWALI_No11: Hadi sasa kampuni ya ABN360 imeshatoa tuzo za "Forbes Africa POY Awards" mara ngapi?
JIBU: Hadi sasa kampuni hii imetoa tuzo hizi mara 4. Walianza mwaka 2012, kisha 2013, 2014, 2015, na sasa 2016. Mwaka huu ni mara ya 5.

#WALI_No12: Je washindi wa tuzo hii tangu ianze kutolewa ni akina nani?
JIBU:
2012: James Mwangi, COE wa Equity Bank ya nchini Kenya.
2013: Akinwumi Adesina, Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Africa (ADB). Huyu zamani alikuwa Waziri wa Kilimo nchini Nigeria kwahiyo tusichanganyikiwe niliposema tuzo hizi si za wanasiasa. Alipewa tuzo kwa mchango wake ADB.
2014: Aliko Dangote, CEO wa Dangote Group (Nigeria).
2015: Mohammed Dewji, CEO wa METL (Tanzania).

Ukiangalia orodha hiyo hapo juu utaona hakuna mwanasiasa aliyewahi kushinda.  Kwahiyo hii ni mara ya kwanza mwanasiasa kupewa nafasi kubwa ya kushinda (kama matokeo yatabaki yalivyo).
#SWALI_No13: Tuzo hii ilianzishwa kwa malengo gani?

JIBU: Tuzo hii ilianzishwa kwa ajili ya kuwatambua wafanyabiashara au watu ambao si wafanyabiashara lakini wameweza kuwa na ushawishi wa kibiashara na kukuza sekta ya biashara kwenye zao jamii zao, licha ya vikwazo mbalimbali walivyokutana navyo.

Ukisoma tovuti rasmi ya tuzo hizi (ingia hapa www.poy2016.com) wanasema "Person of the Year Awards 2016, is for the individual who, for better or worse, has had the most influence on business on the year gone by”
Kwahiyo kwa mujibu wa waandaaji wenyewe, tuzo hizi ni kwa ajili ya wajasiriamali na wafanyabiashara, na SI KWA AJILI YA WANASIASA. Unless wanasiasa hao wawe wamekua na influence ya kustawisha biashara katika maeneo yao.

#SWALI_No14: Ikiwa LENGO KU la tuzo hizi ni kurecognize wafanyabiashara/wajasiriamali au watu wengine wasio wafanyabiashara, lakini wameweza kukuza sekta ya biashara katika jamii zao, je wanasiasa waliopendekezwa mwaka huu wana mchango wowote mkubwa katika biashara kwenye jamii zao?
JIBU: Hapana. Kwa maoni yangu si JPM wala Bi.Gurib (Rais wa Mauritania) mwenye mchango wa "kueleweka" wa kukuza biashara katika nchi zao. Zaidi sana hapa kwetu tumeona biashara zikizidi kuporomoka badala ya kustawi. Tumeona mahoteli yakifungwa, mabenki yakifilisika, bidhaa zikikosa soko, na wafanyabiashara wakikosa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji yao. Sasa tujiulize, je tuzo hizi zinatolewa kwa waliokuza biashara au waliozorotesha biashara?

#SWALI_No15: Je tuzo hizi zimewahi kutolewa kwa Mwanasiasa?
JIBU: Hapana. Hazijawahi kutolewa kwa mwanasiasa. Wapo wanasiasa ambao wamewahi kupendekezwa lakini hawakushinda. Mwaka jana Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alipendekezwa lakini akaangushwa na Mohammed Dewji, CEO wa METL.

#SWALI_No16: Kwanini wanasiasa "wengi" wanakua nominated kwenye tuzo ambazo haziwahusu moja kwa moja?
JIBU: Mfumo wa kupendekeza "nominees" upo VERY WEAK. Ni mfumo ambao mtu yeyote mwenye "smart phone" au "computer" anaweza kuingia na kupendekeza jina la mtu yeyote anayemtaka then wale waliopendekezwa mara nyingi ndio wanateuliwa kuwa "nominees". Kwahiyo kuna "loophole" ambayo inaweza kutumika vibaya. Wanasiasa wanaweza kuajiri watu wa kuwanominate. Ingia hapa uelewe nachosema http://poy2016.com/

#SWALI_No17: Je jarida la Forbes ambao ni owner wa jina linalouza tuzo hizi wameruhusu wanasiasa kuwa nominated?
JIBU: Mkataba ambao kampuni ya ABN360 imeingia na jarida la Forbes unahusu kurecognize wafanyabiashara au mtu aliyefanya jambo kubwa kwenye biashara na maendeleo ya uchumi (hata akiwa mwanasiasa). Forbes ni jarida maalumu la masuala ya biashara na uchumi, kwahiyo kitendo cha kampuni ya ABN kuingiza wanasiasa (ambao hawana mchango wa maana kwenye biashara) kinaweza kuathiri mkataba kati ya Kampuni ya ABN360 na Forbes Inc. Ikiwa Forbes watahisi kipengele chochote cha mkataba kuvunjwa, huenda wakazuia jina lao lisiendelee kutumika tena kwenye tuzo hizi.

#SWALI_No18: Je ni kweli JPM anaongoza kwa kura miongoni mwa "nominees" wa mwaka huu?
JIBU: Hadi sasa matokeo yanaonesha hivyo. Zoezi la upigaji kura limesitishwa huku JPM "akiaminika" kuongoza kwa 84% akifuatiwa na Jamhuri ya watu wa Rwanda iliyopata 12% ya kura zote.

#SWALI_No19: Je zoezi la upigaji kura ni huru na justifiable kisheria?
#JIBU: Ni ngumu sana kujustify uhalali wa kura walizopigiwa nominees kwa sababu zoezi la upigaji kura liliruhusu mtu mmoja kupiga kura zaidi ya mara moja kwa siku moja. (Ingia hapa ujionee mwenyewe http://poy2016.com/).
Mtandao uliokuwa ukihesabu kura uliruhusu mtu mmoja kupiga kura kwa wingi kadri iwezekanavyo. Unachofanya ni kupiga kura, then unafunga hiyo page halafu unafungua upya na kupiga tena. Kwahiyo inawezekana kuna watu walipiga kura hata mara 50 au 100 kwa siku. Katika mazingira yenye OMBWE KUBWA kiasi hiki huwezi kusema kura zote zilikua halali. Huenda waliajiriwa vijana maalumu kufanya kazi ya kuwapigia kura "watu wao."

#SWALI_No20: Je JPM anastahili kushiriki tuzo hizi? Ni za hadhi yake?
JIBU: Kwa maoni yangu tuzo hizi hazina hadhi ya kushindaniwa na Rais wa nchi. Ni tuzo za wajasiriamali. Nilitegemea kuona akina Mengi, Bakhresa, au mzee Sabodo wakipendekezwa kuwania tuzo hizi na sio 

"Mheshimiwa Rais". Kwangu mimi sioni fahari hata kidogo Rais kushindania tuzo za wajasiriamani. Ningejisikia fahari kuona "Rais wangu mwema" akishiriki tuzo kubwa kama "NOBEL" au tuzo za kiongozi bora Afrika (MO Ibrahim Awards), lakini sio kwenye tuzo hizi ya wajasiriamali.

Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema Ukweli.

Malisa GJ | Your Partner In Critical Thinking.!

1 comments:

You know your projects stand out of the herd. There is something special about them. It seems to me all of them are really brilliant!
event production agencies in dubai