POLISI WAPEWA RUNGU KUWASHUGHULIKIA WAHALIFU

Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema amewaagiza Polisi kutumia nguvu zote kupambana na watuhumiwa wa uhalifu.

Hata hivyo, alisema amelionya jeshi hilo kuangalia baadhi ya makosa na adhabu wanazotoa ikiwamo kuwakamata na kuwafikisha mahakamani vijana au kuwaweka mahabusu wakichanganyika na watu wazima wenye makosa ya kihalifu. Waziri alisema vitendo vya aina hiyo si  sahihi.

Nchemba alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu swali la Fakharia Shomar Khamis (Viti Maalumu -CCM) aliyetaka kujua Serikali inatoa tamko gani kuhusu usalama wa askari wake. “Mpaka sasa Serikali imekamata silaha ngapi zilizoporwa kutoka kwa askari waliovamiwa wakiwa wanatekeleza majukumu yao,” alihoji mbunge huyo.
#Mwananchi