AMCHOMA MFANYAKAZI WAKE WA NDANI KISA KACHELEWA KUPIKA MBOGA

Jeshi la Polisi Jijini Mbeya linamshikilia mfanyaiashara mmoja mkazi wa Uyole kwa tuhuma za kumwagia mafuta ya moto mfanyakzi wake wa ndani.



Mtuhumiwa huyo ambye ni mfanyabiashara wa minada na mkazi wa uyole anadaiwa kumchoma kwa mafuta mfanykazi wake huyo kwa kosala kuchelewa kupika mboga.

Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Dhahir Kidavashar alisema kwamba mtuhumiwa alikamatwa juzi nyumbani kwake baada ya kumuwekea mtego kwa kumsaka kwa siku kadhaa bila mafanikio
Mama mdogo wa Binti huyo witness Mgaya amesema mwanae anaendelea vizuri ila wanakabiliwa na uhaba wa fedha za dawa na chakula.

Kwa mujibu wa maelezo ya binti huyo, alifika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo mwezi machi mwaka huu na kuanza kazi za ndani na hajawahi kulipwa ujira wake muda wote huo.

Alisema siku ya tukio mtuhumiwa alirudi jioni kutoka kazini na kuanza kumtuhumu kuwa amechelewa kupika mboga hivyo alichukua mafuta ya kupikia yaliyokuwa jikoni na kumwagia.