WATOTO KUZALIWA NA WAZAZI WATATU UINGEREZA

Serikali nchini Uingereza imeidhinisha shughuli ya kimatibabu ambayo itawezesha watoto kuzaliwa na wanawake wawili na mwanamume mmoja.



Uamuzi huo wa kihistoria unatokana na uvumbuzi wa kisayansi ambao unalenga kuzuia watoto kuzaliwa wakiwa hawana matatizo ya kurithi kutoka kwa wazazi hao.

Madaktari Newcastle - waliovumbua aina hiyo mpya ya IVF (njia ya kutungishia mayai mbegu nje ya mama na kuyarejesha katika mji wa uzazi) - wanatarajiwa kuwa wa kwanza kutoa huduma hiyo kwa na tayari wametoa wito kwa watu wanaotaka kutoa mayai kujitokeza.Mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa njia hiyo anatarajiwa mwishoni mwa mwaka 2017.Baadhi ya familia zimewapoteza watoto kadha kutokana na matatizo yasiyoweza kutibiwa, ya cha chembe zilizo ndani ya seli ambazo hufahamika kama mitochondria, yanayotokana na chembe za kinasaba au jeni. Baadhi ya matatizo haya ya kiafya yanaweza kuwaacha watu wakiwa hawana nguvu ya kuufanya moyo kuendelea kupiga na hivyo kufariki.

#BBC