WAFARIKI PAPO HAPO KWA AJALI YA BASI

Watu 3 wanasadikika ku fariki dunia na wengine 13 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Ngasamo Express kupata ajali Mafindi Iringa usiku wa kuamkia leo.



Ajali hiyo imetokea eneo la Kinyanambo C, ambapo basi la abiria la kampuni ya Ngasamo Express liliacha njia na kupinduka.

Majeruhi wote wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi iliyopo mjini Mafinga na miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti Hospitalini hapo.