LOWASA ASIFIA UTEUZ WA RAIS MAGUFULI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amepongeza uteuzi uliofanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli ambapo alimteua Dk. Emmanuel Nchimbi kwa Balozi.



Edward Lowassa aliyekuwa miongoni mwa watia nia wa Chama cha Mapunduzi alisema kuwa ni jambo jema kushirikisha viongozi kuongoza nchi huku akibainisha kuwa mbali na uteuzi wa Dk. Nchimbi pia kuteuliwa kwa mabalozi wengine nako kumemfurahisha.

Wakati Lowassa akisifia uteuzi wa Dk. Nchimbi, wachambuzi wengine wa masuala ya kisiasa walisema kuwa uteuzi huo unalenga kumaliza mvutano wa muda mrefu na mgogoro ulioibuka ndani ya CCM wakati chama hicho kikitafuta mgombea atakaye peperusha bendera yake katika uchaguzi mkuu mwaka jana.

Dk. Nchimbi ni mwanachama wa CCM ambaye alikuwa ni mwanamkakati katika kambi ya Lowassa wakati wa mbio zake za kuwania kuteuliwa na chama hicho kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Lowassa aliaema kuwa Dk. Nchimbi alikuwa akionekana kama msaliti ndani ya chama hicho, lakini anaamini kufuatia uteuzi huu shutuma hizo zitapungua. Aidha, alimsifia Dk. Nchimbi na kusema ni kiongozi mwenye uzoefu.