MWILI WA FIDEL CASTRO KUCHOMWA MOTO

Cuba inaadhimisha siku tisa za maombolezo kufuatia kufariki kwa Fidel Castro, anayejulikana kwa siasa zake za kimapinduzi, aliyetawala taifa hilo kwa miongo kadhaa na ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 90.



Mwili wake, utachomwa hadi kuwa majivu kama alivyotaka, katika sherehe ya kibinafsi, ambapo majivu yake yatazungushwa katika msafara maalumu kote nchini kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mji wa Santiago Desemba tarehe nne.

Akiwa kiongozi mwenye mrengo wa kushoto na mwanamapinduzi msifiwa, alipendwa na kuchukiwa na watu mbalimbali kote duniani.