Shamsa Ford awaasa Wanawake wenzake kuhusu kupunguza Chuki na Matusi
























Shamsa kayaongea haya kwa Wanawake wenzie 

Natamani ifike siku wanawake tukomae kiakili na kuua ile kauli wanayosema watu kwamba mwanamke ni mdhaifu...ila hatuwezi kufikia malengo kama sisi wanawake wenywewe hatupendani. Wanaweka tunaonea wivu.
Ukiona mwenzio amekupita kitu eti unamuonea wivu na kumuwekea roho mbaya badala ya kumuweka karibu na ujifunze jinsi alivyofanikiwa ili na ww ufanikiwe .WANAWAKE wengi tunapoteza muda kwa kuwa na vigenge au vikundi vya marafiki ambao muda mwingi mnatumia kusengenya na ujinga tu badala ya kudiscuss maendeleo,tunapoteza muda mwingi kwa mashindano ya kijinga ambayo hayana faida yoyote katika MAISHA YETU .
WANAWAKE  wengi sana wana akili za kitoto muda mwingine.Ukiona wanawake wenzako wamegombana badala ya kutafuta njia ya kuwasuruhisha wewe ndo kwanza unapigilia nyundo  kwa juu.Sasa unafaidika nini?MWANAMKE anaweza akatumia nguvu zake zote ili kuweza kumuumiza mwanamke mwenzie bila hata huruma kwamba ni mwanamke kama yeye.
WANAWAKE JAMANI tukumbuke kwamba sisi tunakua haraka na kuzeeka HARAKA ..MWANAUME anaweza akafikisha miaka 55 na akaoa katoto .ila SISI WANAWAKE TUKIFIKISHA miaka 45 tu TUSHAGOTA .hata humu insta ukichunguza sana WANAWAKE NDO TUNAONGOZA kwa chuki na matusi kwenye page za wenzetu badala ya kutiana moyo ili kuleta MAENDELEO.
WANAWAKE WENZANGU TUTUMIE MUDA WETU VIZURI KATIKA KULETA MAENDELEO KATI YETU NA INAWEZEKANA.TUSICHEZE NA MAISHA IPO SIKU YATATUDAI KODI. WANAWAKE OYEEEEE