Diamond na Team nzima ya Wasafi kushiriki kupanda Mti #Oct1st



Maneno ya Diamond kukiri kushiriki tarehe 1 octoba katika siku yakupanda Mti kwenye Kampeniya Mti Wangu..............Haikuwa rahisi kuhairisha show yetu ya #Oct1st lakini ki hali ya ubinaadam hatukuweza kabisa kuendelea kutangaza show ama sherehe yetu ya  #Oct1st ilhali Wenzetu wa Bukoba hivi karibuni wamepatwa na tatizo na still wapo tatizoni..... hivyo tukaonelea kihekima ni vyema Kusitisha ama kupeleka mbele show yetu ya #Oct1st.... lakini pia, Kwakuwa Mkuu wa mkoa wetu Mh PAUL MAKONDA anatusihi kila mwana Dar Es Salaam tareh 1 ya Mwezi wa kumi kila mtu kupanda mti katika Eneo Lake.... basi nasi kama WCB tukaamua siku hii #Oct1st tuitumie katika kumuunga mkono Mkuu wa mkoa na Kuhakikisha sisi na team zetu zote tunakuwa Mstari wa Mbele Kutoa taarifa na kuhakikisha tuna panda miti ili kuboresha ama kupendezesha  Nchi yetu pendwa..... Tafadhali share habari hii ili wote tupate taarifa na Tareh Moja tupande miti katika maeneo yetu....shukran🙏 #MtiWangu