JINA LA ROMA LAWA GUMZO TENA BAADA YA KUTOA KIPANDE CHA VIDEO MTANDAONI AKIIMBA WIMBO WA DINI


Msanii wa muziki wa hip hop Roma Mkatoliki
amekuwa gumzo baada ya kuonekana akiimba wimbo wa kumsifu Mungu ikiwa na wiki moja toka atekwe na kuachiwa.

Katika video hiyo rapa huyo amelalamika jinsi watu wanavyomsema vibaya kutokana na matatizo hayo ambayo yalimkuta akiwa na wenzake watatu.

Roma alisisika akisema “Ninalalaa macho wazi mimi, kama ndege mkiwa juu ya paaa, Nimekuwa kama muhuni mimi, fanya ima, fanya ima bwana uniokoee. Nimekuwa kama kichekesho kwa watu mimii bwanaa, kila nipitapo kunisema nakunicheka, munguu wangu mbona umeniachaa,”

Rapa huyo na wezake walitekwa na watu wasiojulikana wakiwa Tongwe Record na baadaye kutelekezwa katika beach za Uninio Jijini Dar es salaam.