Ofisi ya Bunge la Muungano imependekezwa ichunguzwe na TAKUKURU



Ofisi ya Bunge la Muungano na TCRA ni miongoni mwa taasisi 9 ambazo Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imependekeza zichunguzwe na TAKUKURU baada ya kuonyesha viashiria vya rushwa.

Haya yanakuja ikiwa hivi karibuni Bunge lilitangaza kubana matumizi na kuweza kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 6.