Serikali Zanzibar imewasilisha marekebisho ya Katiba ya Zanzibar



Serikali Zanzibar imewasilisha marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ambayo yatampa uwezo Rais wa Zanzibar, kuchagua wajumbe wa Baraza la Wawakilishi bila ya kushauriana na Kiongozi wa Upinzani.

Katiba ya Zanzibar ilikuwa ikimtaka Rais wa Zanzibar kushauriana na Kiongozi wa Upinzani kabla ya kufanya teuzi za Baraza la Wawakilishi.