MKUU WA MKOA MTWARA AWASHUSHA VYEO WALIMU 63

Mtwara: Baada ya Mtwara kushika nafasi ya pili kutoka mwisho nchini, Mkuu wa Mkoa Huo, Halima Dendego amemwagiza Katibu Tawala mkoa kuwavua madaraka walimu wakuu 63 wa shule za msingi ndani ya masaa 24.

Halima Dendego


Pia ameagiza kuvuliwa kwa madaraka maofisa elimu wa shule za msingi wa halmshauri za Tandahima, Nanyumbu, Newala na Mtwara Vijijini.

Wengine watakao guswa na adhabu hiyo ni baadh ya waratibu kutoka Halmashauri za Masasi , Manispaa ya Mikindani, Mtwara vijijini, Nanyumbu, Newala na Tandahimba.

Akizungumza jana katika kikao cha watendaji, alisema wamefikia uamuzi huo baada ya shule hizo kufaulisha chini ya wastani wa asilimia 50 sambamba na kuwepo udanganyifu.

Dendego alisema katika matokeo ya mwaka jana mkoa huo ulishika nafasi ya 12 kitaifa na baadhi ya Wanafunzi walichaguliwa kwenda za vipaji maalumu lakini walibainika kuwa hawajui kusoma na kuandika.

“Tulipopata ishara ya udanganyifu tulikubaliana kubadilisha mtindo wa usimamizi wa mtihani na kweli mwaka huu matokeo tumeyaona, wanaofaulu ukweli tumewaoona na wanaofaulu kwa udanganyifu tumewaona. Haiwezekani shule ikawa miaka miatatu mfululizo ya kwanza kimkoa, leo baada ya kuweka vizuri maswala ya usimamizi ikawa 160. Ile orodha ipo ijumlishe na wale wakuu wale wote wavuliwe madaraka, NAAGIZA” alisema Dendego.

Chanzo #Mwananchi