RAIS WA GAMBIA YAHYA JAMMEH AKUBALI MATOKEO BAADA YA KUSHINDWA NA MPINZANI WAKE KWENYE UCHAGUZI

Rais Yahya Jammeh wa Gambia ambaye ameliongoza taifa hilo la magharibi mwa Afrika kwa miaka 22, amekubali kushindwa na mpizani wake, Adama Barrow, kwa mujibu wa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Alieu Momar.

Rais wa Gambia


Yahya Jammeh alikuwa akiwania wadhifa huo kwa mara ya tano kupitia chama chake cha Alliance for Patriotic Reorientation and Construction (APRC) amesema kuwa atahutubia taifa na kumpongeza Adama Barrow aliyeibuka mshindi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Alieu Molar Njie ametangaza matokeo ya mwisho na kubainisha kuwa mshindi wa nafasi ya Urais Adama Barrow amepata kura 263,515 na Yahya Jammeh kura 212, 099.

Rais Yahya Jammeh amekubali matokeo hayo ikiwa ni baada ya kutawala taifa hilo la Afrika Magharibi kwa miaka 22.