SERIKALI YABARIKI YANGA KUTUMIA UWANJA WA TAIFA KAMA UWANJA WAKE WA NYUMBANI

Serikali imesaini Mkataba na Yanga utakaoiruhusu klabu hiyo kuutumia Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Uhuru katika michezo yake ya Kitaifa na ya Kimataifa.

Yanga


Miongoni mwa masharti ya Mkataba huo ni endapo kutatokea uharibifu wowote utakaofanywa na wachezaji ama mashabiki, Klabu hiyo itabeba gharama za matengenezo.

Mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Serikali na Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Bwana Baraka Deusdedit.