Mwanasheria Mkuuu wa Zanzibar aliefukuzwa baada ya Bunge la Katiba apata Kazi Umoja wa Mataifa

Anaandika #Ismail_Jussa,

HESHIMA KUBWA KWA OTHMAN MASOUD OTHMAN NA KWA ZANZIBAR

OTHMAN MASOUD OTHMAN 


NI HESHIMA KUBWA kuwaarifu kwamba Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la WIPO (World Intellectual Property Organization) uliofanyika Geneva, Switzerland October 3-11 umemteua Mhe. Othman Masoud Othman kuwa Mjumbe wa Kamati ya Usimamizi ya WIPO (INDEPENDENT OVERSIGHT COMMITTEE) akiwa mwakilishi kutoka Africa katika Kamati hiyo ya watu 7 nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Bibi Mary Ncube kutoka Zambia.

Watu 36 walikuwa shortlisted kugombea nafasi hiyo baada ya kuchujwa kutoka watu 71. Hii sio kazi ya ajira bali ni kama Bodi ya kusimamia nidhamu, uwajibikaji, matumizi ya fedha, ukaguzi wa ndani, uchunguzi wa makosa na kutoa ushauri katika kufukuzwa kazi kwa baadhi ya maofisa wa Shirika hilo la UN. Kamati hukutana kwa siku 5 hadi 7 Geneva kila baada ya miezi 3. Aidha Kamati hufanya vikao na baadhi ya watendaji na maofisa wa WIPO.

Ili kujua zaidi mamlaka na uzito wa chombo hicho tafadhali google WIPO IAOC. Lakini kwa ufupi Kamati inaundwa na wajumbe 7 kutoka kanda 7 za WIPO. Afrika, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Europe, Asia, China special zone na Australia na Pacific mjumbe mmoja kila kanda.

Akizungumzia uteuzi huo, Mhe. Othman Masoud Othman amesema:

"Naamini kwamba uteuzi huu ni heshima kwa Zanzibar na hasa kwa wapigania haki na ustawi wa nchi yetu. Ni kielelezo kwamba dunia inatupa heshima kwa uwezo wetu wa kusimamia uendeshaji wa Shirika nyeti la UN kama WIPO ambalo ndio shirika pekee linalojitegemea kifedha na kuwa na akiba. Wakati wa interview kitu kimoja kilichowavutia wajumbe wa panel ya interview ni majibu yangu kwa suali lao, "What is a single extraordinary thing you have done to show that you are a person of principle and integrity?" Jibu langu lilikuwa ni uamuzi wangu katika Bunge la Katiba wa kusimamia ninachokiamini. Again I take this as an honour to the people of Zanzibar."

HONGERA MHE. OTHMAN MASOUD OTHMAN.
HONGERA ZANZIBAR