Rais ameivunja Bodi ya TRA kwa madai kuwa inapiga deal kwa kuweka pesa za wananchi kwenye Fixed account. Sheria ya TRA ya mwaka 2006, kifungu cha 10 kinaeleza composition ya wajumbe wa Bodi ambao ni:
1. Mwenyekiti (anayeteuliwa na Rais)
2. Katibu mkuu wizara ya fedha (Muungano)
3. Katibu Mkuu wizara ya fedha (Zbar)
4. Gavana wa BOT
5. Kamishna wa TRA
6. Wajumbe wanne wa kuteuliwa na Waziri.
1. Mwenyekiti (anayeteuliwa na Rais)
2. Katibu mkuu wizara ya fedha (Muungano)
3. Katibu Mkuu wizara ya fedha (Zbar)
4. Gavana wa BOT
5. Kamishna wa TRA
6. Wajumbe wanne wa kuteuliwa na Waziri.
MALISA |
Sasa kwa akili ya kawaida Rais kuvunja Bodi bila kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji hapo juu hakuna alichofanya. Maana akiunda Bodi mpya wajumbe watarudi haohao isipokua Mwenyekiti na hao wanne wa kuteuliwa na Waziri. Yani Gavana atarudi huyohuyo, Kamishna atarudi huyohuyo, Makatibu wa wizara wote watarudi maana wanaingia kwa nafasi zao.
Ambao hawatarudi ni Mwenyekiti na wale wanne wakuteuliwa na Waziri tu. Katika mazingira haya ni rahisi watu kufikiria kwamba huenda Rais alikua na sababu tofauti na aliyoieleza. Mtu anaweza kufikiria huenda issue sio "fixed a/c", huenda issue ni Mwenyejiti wa Bodi. Namna pekee ya Rais kuprove kwamba Bodi nzima ilikua "hovyo" ni kuwafukuza kazi wajumbe wa bodi wanaoingia kwa status zao. Amfukuze kazi Gavana wa BOT, Makatibu wakuu na Kamishna TRA. Ili akiunda Bodi mpya waingie watu wote wapya. Vinginevyo sioni sababu ya Rais kuivunja Bodi. Elimu, Elimu, Elimu.!
Malisa GJ