MTOTO WA DONALD TRUMP ALINDWA NA KIKOSI CHA ASKARI 150 AKIWA UFUKWENI

Ulinzi kwa familia ya Rais mteule Donald Trump ameonekana kwa mara ya kwanza hadharani wakati maofisa usalama wakiwa na silaha nzito wakimlinda mmoja wa watoto wa kiongozi huyo alipokuwa akicheza ufukweni na wenzake.



Mtoto huyo Barron Trump (10) anayesoma katika shule moja mjini New York, hivi karibuni alikuwa ameambatana na watoto wenzake kushiriki michezo iliyoeleza kuwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku shukrani

Akiwa katika michezo ya kawaida mtoto huyo alionekana kuzungukwa na askari waliokuwa na silaha malimbali kwenye boti iliyokuwa ikipiga doria.

Baadhi ya askari hao mbao walikuwa wamevalia kiraia muda wote walionekana kuwa makini kumfuatilia mtoto huyo.

Ripoti zinasema kuwa timu ya askari 150 ilipewa jukumu la kuilinda familia hiyo ambayo ilionekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa matokeo ya uchaguzi uliopita.
Wakati wote wa tukio hilo mtoto huyo alizungukwa na askari watatu huku wengine wakiwa pembeni

Boti iliyokuwa na silaha nzito ailionekana ikizunguka huku na kuke lakini lakini ilihakikisha haitoki mbali na eneo ambalo mtoto huyo alikuwa na wenzake.

Macho yote ya askari yalikuwa yameelekezwa kwa mtoto huyo ambaye ataendelea kuishi mjini New York na mama yake wakati Trump atahamia Washngton kuanza kutekeleza majukumu ya urais.

Chanzo: BBC