TANGAZO ALILOWEKA MZEE ATHUMAN (75) AKIELEZA SIFA ZA MKE ANAYEMTAKA

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 75 anayeishi eneo la Mbagala, Dar es Salaam nchini Tanzania ameweka tangazo kando ya barabara kwenye mtaa anaoishi lenye sifa za mke anayemtaka.



Mzee Athuman Bakari Mchambua akizungumza na BBC alisema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kifiwa na mke wake. Alieleza kuwa hawezi kutumia njia nyingine yoyote isipokua udahili ama mahojiano kumpata mke.

Miongoni mwa sifa alizozitaja katika tangazo hilo la kutafuta mke alisema kuwa awe mwenye kushika dini, mvumilivu wa ndoa, mwenye uwezo wa kulima na anyempenda mumewe.

Hadi sasa amesema kuwa amefanya mahojiano na wanawake wanne lakini hakuna aliyetimiza vigezo alivyoviweka ambapo alisema kuwa wengi walikuwa na sifa mbili tu.

Mtoto wake wa kike Dalia Mchambua alisema kuwa anaunga mkono hatua hiyo iliyochukuliwa na baba yake na kuwa atamkubali yeyote atakayeshinda awe mama yake.