KINANA AOMBOLEZA KIFO CHA PROFESA MTULIA

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CCM Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Mwishehe Shaban Mlao kufuatia kifo cha Profesa Idrissa Ali Mtulia, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Rufiji.



Profesa Mtulia alifariki jana nyumbani kwake jijini Dar es salaam.Profesa Mtulia ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali.

Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Katibu Mkuu wizara mbalimbali, Daktari wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili na Mwenyekiti wa Bodi ya Madawa (MSD)

“Atakumbukwa na wanachama wa CCM na Wananchi wa Mkoa wa Pwani kwa jitihada zake za ujenzi na uimarishaji wa Chama na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Wananchi wa Rufiji.” Alisema Kinana katika taarifa iliyoletwa na CCM