Diwani Asiyejua Kusoma Wala Kuandika Asimamishwa Baada ya Kutohudhuria Vikao Tangu Disemba
Diwani asiyejua Kusoma |
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita limemsimamisha Diwani wa Kata ya Senga Joel Ntinginya kutoendelea na nafasi yake baada ya kutohudhulia vikao vya baraza tangu kuapishwa kwake Disemba mwaka jana.
Diwani huyo amekuwa akituhumiwa kutokujua kusoma wala kuandika.
Baada ya kupoteza sifa ya kuendelea kuwa Diwani wa Kata ya Senga, mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita amesema tayari ameshapeleka barua TAMISEMI kwa ajili ya hatua zaidi.