Mwanasiasa Mkongwe, Stephen Wassira aliyeshindwa katika kesi yake ya Uchaguzi dhidi ya Mbunge Ester Bulaya(CHADEMA) amesema kuwa hajastaafu siasa na mwaka 2020 atagombea tena.
Alipopigiwa simu leo mchana na kituo kimoja cha runinga na kuulizwa maoni yake kuhusu hukumu ya kesi yake ya uchaguzi, amedai ameshtushwa sana na hukumu hiyo ambayo aliona alikuwa na kila dalili ya kushinda.
Alipoulizwa nini malengo yake kama ameamua kuwekeza kwenye kilimo au uvuvi alisema yeye maisha yake yote hajui chochote zaidi ya siasa, na ni wakati wa Bulaya kujiandaa na lolote maana anataka 2020 awatumikie wana Bunda "nitamgalagaza vibaya sana binti Bulaya" na pia akasisitiza siasa hawezi kustaafu leo wala kesho.