ZAHANATI NCHINI INDIA YAJITOLEA KUMSAIDIA BARAKA BAADA YA HOSPITALI YA MUHIMBILI KUSHINDWA KUTIBU KUTOKANA NA UREFU WAKE

Wakati mgonjwa Baraka Elias akisubiri hatima ya matibabu yake yaliyoshindikana katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) kutokana na urefu wake, zahanati moja nchini India imejitolea kumsaidia kufanyiwa upasuaji nchini Tanzania.



Daktari katika zahanati ya Speedy Recovery, Dk Shaila Raveendran amekaririwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa wanaweza kumsaidia Elias ambaye madaktari wa Moi wanasema hakuna vifaatiba vinavyolingana na mifupa yake.

Elias mwenye Urefu wa futi 7.4 au mita 2.20, anahitaji kufanyiwa upasuaji baada ya kuanguka

#Mwananchi