LUKUVI AWAANIKA MATAPELI 30 WA ARDHI



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amekabidhi polisi majina ya watu 30 wanaodaiwa kuwa matapeli wa ardhi ili washughulikiwe.



Waziri Amesema kuwa amekabidhi majina hayo kwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro ambaye alithibitisha kupokea majina hayo na kwamba tayari yameshafunguliwa majalada kwa ajili ya upelelezi.

“Ni mapema mno kuzungumzia jambo hili, kwa sababu lipo kwa wapelelezi. Ni kweli majina haya tumeyapokea na tayari majalada yamefunguliwa,” alisema.