GEITA: MVUA YABOMOA NYUMBA 236 CHATO



Tathmini ya Halmashauri imesema kuwa mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Novemba 1 imebomoa nyumba 236 na kuziacha Kaya 38 zikiwa hazina makazi.


Aidha mvua hiyo imewajeruhi watu 23 ambao ni wakazi wa Kata ya Ilyamchele. Mkuu wa Wilaya amemtaka Mhandisi wa ujenzi kupiga kambi katika eneo hilo ili ahakikishe kuwa maeneo hayo yanahimarika kimiundombinu.