Desturi ya kudai mahari kutoka kwa MTU anaetaka kuoa ni utamaduni na mila za kale zinazoendelea miongoni mwa watu na makabila mengi duniani. Kwa asili mahari ilikuwa ni dhamana kwamba atakayeolewa atathaminiwa na kuhesabiwa kuwa Mke halisi na hivyo kutendewa vizuri, kwa kadri mahari ilivyokuwa kubwa,ndivyo Mke alivyojiona wa thamani zaidi. Lakini mambo yanatakiwa kubadilika, Msingi wa ndoa ni Upendo .Upendo huo ni wa thamani kubwa sana na wa kudumu kuliko mifugo, pesa au vitu vyovyote vitolewavyo kama mahari.
Hivyo watu wanao mjua Mungu wanaoana kwa Upendo wa kweli hawana haja ya kuwa na dhamana nyingine ya usalama wa ndoa yao. Inashangaza na kusikitisha kuona baadhi ya wazazi hudai mahali kubwa ili kujipatia mali kupitia watoto wao. Mahari kubwa sana hudaiwa kwa anaetaka Kuoa. Na ndo mana Vijana wa sikuhizi wengi wanachelea kuoa kwa sababu inawachukua takribani miaka mitatu kujipanga kimaisha, na takribani miaka mitatu mingine Kujipanga na mahari na harusi.
Sio Kwamba Mahari zisiwepo, Hapana, bali mahari isiwe kikwazo cha kuwaruhusu wawili waliopendana washindwe kuanza maisha ya Familia, ifike Pahali mahali iangalie na uwezo wa muoaji. Kijana kaenda Ukweni katajiwa Mahari Milioni tatu au Nne, bado Tanzanite ya Engagement, bado hajaambiwa alishe ukweni siku ya Mahari. Akirudi nyuma anakumbuka kuna gauni la kitchen party na send off ya bi harusi, Bado kuna suti yake, gauni la mkewe n nguo za wasimamizi wao. Hapo bado wageni wa mkoani na kuhudumia nyumbani. Akipiga hesabu anajikuta ana Bajeti ya zaidi ya Milioni Saba ndani ya miezi mitatu ya Mahari, Send Off na Ndoa.
Tag waoaji na waolewaji Watarajiwa.
Mwnadishi: Man Deo
Instagram: @elimu_biashara