LOWASSA, SUMAYE, PROF SAFARI WAWAFUNDA WABUNGE WA CHADEMA JINSI YA KUKABILIANA NA HOJA ZA BUNGE



Wabunge wa Chadema wamekutana leo kwenye ukumbi wa St Gasper mjini Dodoma na kupewa mikakati ya namna ya kukabiliana na hoja mbalimbali za vikao vya Bunge vinavyotalajiwa kuanza kesho.

Baadhi ya viongozi wa chama hicho akiwemo aliyekuwa mgombe wa Urais, Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdallah Safari na Profesa Mwesiga Baregu walipata nafasi kuzungumza na wabunge hao na kuwaleza namna ya kupambana wanapokuwa bungeni.

Moja ya ajenda ya mkutano huo ilikuwa ni jinsi ya kukabiliana na mswada wa huduma za vyombo vya habari unaotalajiwa kupitishwa katika mkutano wa tano wa Bunge.