KASSIM MAJALIWA: HATUTAWAVUMILIA WAAJIRI WASIOTOA MIKATABA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitawavumilia waajiri ambao hawatoi mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao na amewaonya waache tabia hiyo mara moja. “Nitoe wito kwa waajiri wote ambao wamekuwa na tabia ya kutokutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao, waache tabia hiyo mara moja, kwani Serikali haitamvumilia mwajiri wa namna hii,” alionya.

Kassim Majaliwa

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Novemba 23, 2016) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere ulioko Chuo cha Mipango, nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Akijibu hoja ya waajiri kutokutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi ambayo iliibuliwa kwenye risala yao, Waziri Mkuu amesema kifungu cha 14 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004  kinaelekeza aina mbalimbali za mikataba inayotakiwa kutumika kuajiri wafanyakazi. “Kisheria mwajiri anao wajibu wa kuhakikisha kila mtumishi wake ana mkataba wa kazi kwa maandishi,” alisisitiza.

“Pia ninawaagiza maafisa wa kazi wanaohusika na kaguzi za kazi kote nchini, wahakikishe kila mwajiri anafikiwa wakati wa ukaguzi na hatua stahiki zinachukuliwa kwa wote wasiotekeleza matakwa ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini,” alisisitiza.

Alisema mkataba wa ajira ni haki ya mfanyakazi na ndiyo ufunguo wa mahusiano mema yanayoweza kuleta utulivu, amani, kuongeza tija na uzalishaji sehemu ya kazi COTU –Kenya yasema wanatamani Rais Magufuli aende kwao kwa mwaka mmoja.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitawavumilia waajiri ambao hawatoi mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao na amewaonya waache tabia hiyo mara moja. “Nitoe wito kwa waajiri wote ambao wamekuwa na tabia ya kutokutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao, waache tabia hiyo mara moja, kwani Serikali haitamvumilia mwajiri wa namna hii,” alionya.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Novemba 23, 2016) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere ulioko Chuo cha Mipango, nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Akijibu hoja ya waajiri kutokutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi ambayo iliibuliwa kwenye risala yao, Waziri Mkuu amesema kifungu cha 14 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004  kinaelekeza aina mbalimbali za mikataba inayotakiwa kutumika kuajiri wafanyakazi. “Kisheria mwajiri anao wajibu wa kuhakikisha kila mtumishi wake ana mkataba wa kazi kwa maandishi,” alisisitiza.

“Pia ninawaagiza maafisa wa kazi wanaohusika na kaguzi za kazi kote nchini, wahakikishe kila mwajiri anafikiwa wakati wa ukaguzi na hatua stahiki zinachukuliwa kwa wote wasiotekeleza matakwa ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini,” alisisitiza.

Alisema mkataba wa ajira ni haki ya mfanyakazi na ndiyo ufunguo wa mahusiano mema yanayoweza kuleta utulivu, amani, kuongeza tija na uzalishaji sehemu ya kazi.