Katika kikao kijacho cha Bunge, Serikali inakusudia kupeleka bungeni na kusoma kwa mara ya kwanza Muswada wa Sheria ya msaada wa Kisheria (The Legal Aid Bill), ambao pamoja na mambo mengine utaruhusu watu wasio na taaluma ya sheria lakini wenye uzoefu na masuala ya kisheria (Paralegals) kutoa msaada wa kisheria, kwa mujibu wa kifungu cha Kifungu 10(1)d(ii) na (iii).
Maana yake ni kwamba ikiwa muswada huu utapita na kuwa sheria, it means wale watu wasio na taaluma ya sheria lakini wanajishughulisha kwa namna moja au nyingine na mambo ya kisheria (mnawaita Bush Lawyers) watatambulika rasmi na watapewa fursa ya kutoa msaada wa kisheria katika baadhi ya masuala ya kijamii.
Nini maoni yako??
MALISA GJ
MALISA GJ