By Malisa GJ,
Rais John Pombe Magufuli ameangushwa katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo za Forbes Person of the Year 2016. Mshindi wa tuzo hizo aliyetangazwa usiku huu ni Bi.Thuli Madonsela, Mkurugenzi wa zamani wa mashtaka nchini Afrika Kusini. Katika tuzo hizo zilizokua na washindani watano, Thuli amewashinda marais wawili wa Afrika ambao ni Rais Magufuli na Rais Ameenah Gurib wa Mauritania.
Thuli ambaye kitaaluma ni mwanasheria anasifika kwa ujasiri wake wa kupambana na makosa mbalimbali hasa rushwa baina ya viongozi na watumishi wa umma. Aliteuliwa na Rais Jacob Zuma mwaka 2009 kuwa Mkurugenzi wa mashtaka nchini humo, nafasi aliyoitumikia hadi October 14 mwaka huu.
Miongoni mwa mambo yaliyompatia umaarufu Thuli ni pamoja na kuibua tuhuma mbalimbali zenye "public interest" ikiwemo skendo ya familia ya Gupta ya kuhonga serikali ili kujipatia nafasi za kisiasa na familia hiyo kumshinikiza Rais Zuma kuteua mawaziri wanaowataka. Kashfa hiyo ni maarufu kama "State of Capture"
Pia Thuli alisimama kidete kuhakikisha Rais Zuma anarudisha kiasi cha dola milioni 16 (takribani bilioni 35 za kitanzania) alizotumia kujenga jumba lake la kifahari huko KwaZulu-Natal. Kashfa hii inajulikana kama "Nkandla scandal"
Thuli ni mama wa watoto wawili (wa kike aitwae Wenzile, na wa kiume aitwaye Mbusowabantu), ambao amewalea peke yake (single parenting) tangu mwaka 1980 mumewe alipofariki na kumuachia watoto hao wakiwa wadogo, huku yeue akiwa mama wa miaka 18 tu. Tangu wakati huo Thuli ameishi mjane kwa kipindi chote cha maisha yake akiwalea watoto hao peke yake.
Thuli Madonsela alizaliwa huko Mbabane Swazilaand mwaka 1962 na kuhitimu masomo yake ya sekondari katika shule ya Evelyn Baring High School. Baada ya kuhitimu alibakia shuleni hapo akiwa kama mwalimu msaidizi (Assistant teacher) na mwaka 1982 alihamia nchini Afrika kusini katika mji wa "makabwela" wa Soweto kutafuta maisha, ambapo aliajiriwa katika shule ya Naledi High School kama Mwalimu Msaidizi.
Baadae alirudi nchini Swaziland kujiendeleza kimasomo ambapo alihitimu shahada yake ya kwanza ya sheria (LLB) kutoka chuo kikuu cha Swaziland mwaka 1987, na kisha shahada ya uzamili ya Sheria (LLM) kutoka chuo kikuu cha Witwatersrand mwaka 1990. Thuli amewahi pia kutunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa sheria LLD (Honoris causa) kutoka chuo kikuu cha Stellenbosch, na chuo kikuu cha Cape Town.
Thuli ana umri wa miaka 54, na alikuwa mwanachama wa chama tawala cha ANC hadi mwaka 2007 alipoamua kujiondoa kwenye siasa za vyama.
#MyTake:
Nichukue fursa hii kumpongeza Thuli Madonsela kwa kushinda. Niwapongeze pia wanawake wote kwa Thuli kuwa mwanamke wa kwanza kushinda tuzo hizi.
Nichukue fursa hii kumpongeza Thuli Madonsela kwa kushinda. Niwapongeze pia wanawake wote kwa Thuli kuwa mwanamke wa kwanza kushinda tuzo hizi.
Binafsi nimefurahi Rais wetu kushindwa kwa sababu mbili,
Mosi; Nilisema tuzo hizi hazina hadhi ya kushindaniwa na "Rais wa nchi". Kwahiyo zingeweza kumshushia hadhi kama angeshinda. Kwahiyo mimi naona ni jambo zuri yeye kushindwa. President has maintained his status. Nadhani ni wakati Rais JPM kujipanga kuwania tuzo zenye hadhi yake. Tuzo za kidiplomasia zenye reputation kubwa kimataifa. Na ili kushinda tuzo hizo itambidi afanye mambo makubwa hapa nchini yatakayomtambulisha vizuri huko nje.
Pili; Nitoe pole nyingi kwa vijana wa Lumumba waliopoteza "bundle" zao na usingizi wao kupiga kura usiku na mchana. Kama JPM angeshinda najua kusingekalika humu ndani. Sasa mtatulia kama kuku aliyenyeshewa mvua, ili iwe fundisho. Otherwise mje na mapovu hapa.
Pia niwasaidie vijana wa Lumumba kwamba ktk tuzo zozote mshindi hapatikani kwa kura tu kama mlivyokua mkidhani. Kuna vigezo vingi zaidi ya kura. Mtu anaweza kuongoza kwa kura lakini vigezo vingine akafeli. Na hiki ndicho kilichotokea kwa JPM. Hadi mshindi anatangazwa JPM ndiye aliyekua anaongoza kwa kura. Lakini kuna vigezo vimemuangusha.
Japo Waandaaji hawajavitaja, lakini tujiulize je ni kukandamiza demokrasia? Je ni kukiuka utawala wa sheria? Je ni kubana vyombo vya habari? Je ni kubana uhuru wa kutoa maoni? Kipi kilichomuangusha JPM? Vijana wa Lumumba tafakarini next time muwashauri wakubwa zenu, badala ya kupoteza "MB zenu za Bundle ya chuo" kupiga kura tu, mkidhani mwenye kura nyingi ndio anatangazwa mshindi kama tuzo za KiliAwards.!
Malisa GJ