MANARA ACHARUKA JUU YA MADONGO YANAYOTUPIWA SIMBA SC

Katika siku za karibuni kumezuka desturi za kuzusha masuala kadhaa ya upotoshwaji hususan kwenye mitandao ya kijamii kuhusu klabu yetu. Desturi hii imeshaota mizizi na inaleta uchonganishi mkubwa baina ya Klabu na wachezaji pamoja na wanachama na washabiki wetu.



kwa kuwa jambo hili la upuuzi linalofanywa mitandaoni ni kuvunja sheria za nchi,klabu imewasiliana na Mamlaka ya mawasiliano nchini(TCRA) na jeshi la Polisi kuona hatua watakazochukua juu ya watu wenye nia ovu na wanaodhani kwa kufanya hivyo wanaiharibu taswira ya klabu yetu,

Tunawaomba Wapenzi wa kandanda nchini puuzeni taarifa zote za mitandaoni ambazo hazikutolewa na idara yangu au mamlaka halali za klabu.

Mwisho niwajuze kwa sasa Simba haijasajili mchezaji yoyote mpya na wala haijamuacha mchezaji yoyote,hadi pale klabu itakapotoa taarifa rasmi,yanayoandikwa huko mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari ni zaid ya porojo.

Imetolewa na Mkuu wa Habari wa Simba Sc.
Haji S. Manara