Upelelezi katika Kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili Salum Njwete(Scorpion) umekamilika.
Hivyo, Mahakama ya Wilaya ya Ilala imepanga Novemba 30, kumsomea maelezo ya awali (PH) mshtakiwa huyo.
Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Flora Haule alipanga tarehe hiyo kwa ajili mshtakiwa huyo kusomewa maelezo ya awali.
Scorpion dar |
Mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na shtaka linalomkabili kutokuwa na dhamana.
Akisoma hati ya mashtaka, Haule alidai Njwete alitenda kosa hilo Septemba 6,mwaka huu eneo la Buguruni Sheli
Alidai siku hiyo ya tukio katika eneo hilo, mshtakiwa aliiba cheni moja ya shingoni aina ya silva yenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili moja ya kiume yenye thamani ya Sh 85,000 , pochi pamoja na fedha taslimu Sh 331,000 na kwamba thamani ya vitu vyote ni Sh 476,000 mali ya Saidi Ally Mrisho.
Kabla na baada ya kutenda unyang'anyi huo, mshtakiwa alimchoma kisu mlalamikaji, machoni na kifuani na kumsababishia upofu wa kudumu.
#mwananchi