MAOMBI YA TANESCO BEI YA UMEME PASUA KICHWA

Ombi la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupandisha bei ya nishati hiyo kwa asilimia 18.19 limeibua mambo mapya baada ya kubainika kuwapo pendekezo la awali la kushusha bei ya umeme kwa asilimia 7.9 mwakani.
Tanesco iliwasilisha maombi mawili kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) Februari 24, ikieleza pamoja na mambo mengine, kusudio la kufanya punguzo la bei ya umeme mwakani.



Ombi jingine lilikuwa ni pendekezo la kushusha bei ya umeme kwa wastani wa asilimia 1.1 kuanzia Aprili Mosi, ambalo lilipitishwa baada ya maoni ya wadau na gharama hizo kupungua kwa asilimia 1.5 hadi 2.4 sambamba na kuondoa gharama za huduma zilizokuwa zinalipwa kila mwezi Sh5,400.

#Mwananchi